25 Apr 2024 / 63 views
Emery asaini mkataba mpya Aston Villa

Kocha wa Aston Villa Unai Emery ameongeza mkataba wake na klabu hiyo hadi 2027.

Villa walikuwa katika nafasi ya 16 kwenye Ligi ya Premia na wakipambana kushuka daraja wakati Mhispania huyo alipochukua mikoba ya Steven Gerrard mnamo Novemba 2022.

Katika mabadiliko ya kushangaza, Emery, ambaye sasa ana umri wa miaka 52, aliiongoza Villa kumaliza katika nafasi ya saba ili kufuzu kwa Ligi ya Mikutano ya Europa, ushiriki wa kwanza wa klabu hiyo katika soka ya Ulaya tangu 2010-11.

Msimu huu, wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England wakiwa na malengo ya kufuzu Ligi ya Mabingwa.

Wako pointi sita mbele ya Tottenham, ambao wana michezo miwili mkononi. Emery alisema yeye na wahudumu wake "wanashiriki maono ya wamiliki na wana muundo sahihi wa kuendeleza klabu hii ya soka".

"Lazima tudumishe moyo wa kufanya kazi kwa bidii, maamuzi ya busara na uratibu na umiliki ambao tumepata wakati huu," aliongeza. "Tutafanya kazi ili kuwa bora na bora zaidi.

Na tutadai kutoka kwa kila mmoja wetu. Tamaa tayari ni, na lazima iwe kauli mbiu ya mradi huu."

Villa wameanzisha chaguo la kuongeza mkataba wa Emery katika hali hii na watakaa na meneja huyo majira ya joto ili kujadili kandarasi ya muda mrefu, BBC Sport inaelewa.

Nafasi ya Emery inaweza kuimarishwa kwa kiasi kikubwa ikiwa atatoa kombe la Ligi ya Mikutano ya Europa na kandanda ya Ligi ya Mabingwa.

Hali ilivyo inapaswa kumaanisha kuwa Villa wanaweza kuona uwezekano wa kuwindwa na Bayern Munich, na pengine vilabu vingine vya Ulaya, kumbakisha meneja wao huko Birmingham.

Emery anayesifika kwa umahiri wake katika mashindano ya Uropa, ameiongoza Villa hadi nusu fainali katika Ligi ya Mikutano, ambapo watamenyana na Olympiakos ya Ugiriki wakiwa na matumaini ya kutinga fainali ya kwanza ya Uropa tangu 1982.